VodaCom

Tangaza na gazeti la Bingwa.

Sunday, November 10, 2013

Tambwe mguu ndani, nje Simba

NA ZAINAB IDDY MSHAMBULIAJI wa Simba, Amisi Tambwe amesema hana muda mrefu kuitumikia Simba, kwani ameanza mazungumzo na timu moja ya Saudi Arabia. Tambwe aliyasema hayo juzi kwenye mazungumzo maalumu saa chache kabla ya kuelekea Bujumbura, Burundi, baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara. Alisema kuna uwezekano mkubwa akavunja mkataba na Simba na huenda asionekane katika kikosi hicho katika  mzunguko wa pili, endapo mazungumzo...

Vita kali ya usajili Simba, Yanga

NA ABDUCADO EMMANUELKITENDO cha Yanga SC kumsajili kipa wa zamani wa Simba SC, Juma Kaseja, kimeonesha kuamsha vita kali ya usajili miongoni mwa timu hizo, lengo likiwa ni kubomoana.Kwa mujibu wa kalenda ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), inaonesha kuwa dirisha dogo la usajili litafunguliwa rasmi Ijumaa ijayo na kufungwa Desemba 15 mwaka huu. Ijumaa iliyopita saa 2 usiku, Yanga ilifanikiwa kuinasa saini ya Kaseja, kwa dau la Sh milioni 40, kwa mkataba wa...

Familia yampeleka Kaseja Yanga

NA EZEKIEL TENDWALICHA ya Juma Kaseja kuwa radhi kujiunga na timu yake ya zamani, Simba baada ya mzunguko wa kwanza kumalizika, kikwazo kikubwa kilikuwa kwa familia yake iliyomtaka kujiunga na Yanga.Familia ya Kaseja ilifikia uamuzi huo baada ya Simba kumtema kipa huyo na nahodha ya timu ya Taifa, ‘Taifa Stars’ kabla ya msimu huu kuanza licha ya kuichezea kwa mafanikio makubwa tangu ajiunge nayo.Tayari Kaseja amesaini mkataba wa miaka miwili Yanga baada ya...

Azam, Coastal Union watunishiana misuli

NA ZAITUNI KIBWANA TIMU za Azam na Coastal Union zinazoshiriki michuano ya Kombe la Uhai inayoshirikisha wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 wa klabu za Ligi Kuu, wametunishiana misuli kwenye michezo ya ufunguzi wa mashindano hayo.Ofisa habari wa Azam, Jafari Iddi aliliambia BINGWA kuwa kikosi chao kimeahidi ubingwa wa michuano hiyo, hivyo Coastal Union wajiandae kwa kichapo.Wakati Jafari akiyasema hayo msemaji wa Coastal Union, Hafidhi Kido alisema kuwa...

Benchi la ufundi Simba kuwasilisha ripoti wiki hii

NA EZEKIEL TENDWARIPOTI ya benchi ya ufundi la timu ya Simba, inatarajiwa kuwasilishwa kwa  kamati ya utendaji wiki hii.Akizungumza jana, Ofisa habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema kuwa makocha wa timu hiyo wameahidi kuwasilisha ripoti kwa kamati ya utendaji wiki ili iweze kufanyiwa kazi.Alisema kwamba baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania bara na timu yao kumaliza wakiwa nafasi ya nne, walitoa muda kwa benchi lao la ufundi...

Kocha Mgambo JKT alia na wachezaji

NA SALMA JUMAKOCHA mkuu wa timu ya Mgambo JKT, Mohamed Kampira ameweka wazi sababu iliyopelekea timu yake kufanya vibaya katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara msimu huu, kuwa ni kuondoka kwa baadhi ya wachezaji wake aliokuwa nao katika ligi iliyopita.Mgambo wanashikilia mkia kwenye msimamo wa ligi hiyo wakiwa na jumla ya pointi 6, baada ya kushinda mchezo mmoja, kutoka sare mechi tatu na kupoteza mechi 9.Akizungumza na BINGWA hivi karibuni, Kampira alisema...

Kung Fu Mbagala kufanya mashindano mara kwa mara

NA ZAINAB IDDYUONGOZI wa klabu ya Kung Fu ya Mbangala jijini Dar es Salaam, umepanga programu ya kufanya mashindano ya mara kwa mara, kwa lengo la kuendeleza mchezo huo nchini.Abdallah Nyoni ni Katibu Mkuu wa klabu hiyo, aliliambia BINGWA kwamba mashindano hayo yatasaidia kupata vipaji ambavyo vitawasaidia katika mashindano mbalimbali.“Hiyo ni moja ya maandalizi ya kuwaandaa wachezaji kwa ajili ya mashindano mbalimbali mwakani, hivyo tunajipanga mapema,” alisema.Alisema...