Sunday, August 4, 2013

Huruma ya kocha yaidhoofisha timu ya makanjanja



Timu ya taifa ya wasichana
KUCHELEWA kwa Bunge kupitisha Muswada wa Sheria ya Udhibiti wa Shughuli za Upangaji Nyumba na Makazi (Rental Housing Act), kunaipotezea Serikali mapato ya mabilioni ya fedha kuliko Sh 1000 ya kodi za kadi za simu (Simcard tax).

Akizungumza na MTANZANIA Jumatano, Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, January Makamba, alisema ni vema sheria hiyo ikaanzishwa haraka ili kuondoa matatizo na lawama kuhusu kodi ndogo ndogo kama za kadi za simu zinazosumbua wananchi.

Makamba, alisema Wizara yake siyo iliyopanga tozo ya kodi hiyo kama baadhi ya wananchi wanavyodhani, kwa sababu haihusiki na kodi ya aina yoyote.

“Sheria ya udhibiti wa shughuli za upangaji, inatakiwa ije haraka kwani ndiyo hasa inayomnyonya mwananchi, kama unafanya kazi na unalipwa mshahara kwa mwezi, kwa nini ulipe kodi ya mwaka mzima, fedha ambayo haiendani na kipato.

“Kenya wanayo sheria hii ambapo mtu ana uwezo wa kulipia nyumba kwa miezi mitatu, kimataifa ni miezi miwili ambapo mtu analipia mwezi wa kwanza na wa mwisho.

“Sheria hii pia itasaidia kuanzishwa kwa mamlaka ya udhibiti wa nyumba kama ilivyo kwenye usafirishaji, ambako kuna Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), kwenye Nishati kuna EWURA, Chakula na Dawa kuna TFDA,” alisema.

Alisema malipo ya kodi ya nyumba kwa mwaka, ndiyo chanzo cha mtu kufanya maovu mengi kama kupokea rushwa, kujiingiza katika biashara ya dawa za kulevya, wizi na mengineyo.

Aidha, Makamba amesema Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, ni mnafiki kwa kukimbilia kutoa namba yake ya simu ya mkononi katika mkutano wa hadhara na kuandika kwenye mitandao, ili wananchi wampigie kumhoji kuhusu uwepo wa kodi kadi za simu wakati yeye mwenyewe alikuwepo bungeni kuipitisha.

“Mnyika ni mnafiki, yeye alikuwepo bungeni na alilijua fika suala hili wala hakusema kitu, baada ya kusikia watu wanalalamika ndiyo anaanza kuongea ongea.

“Ukiona mtu anafanya siasa nje ya Bunge ujue anatafuta umaarufu, kanuni zinamruhusu Mbunge yeyote kupeleka sheria ya mabadiliko, namna ya kubadilisha sheria sio kutoa namba za simu za watu, hizo ni siasa uchwara.

“Rais alishalitolea maamuzi na Serikali inalishughulikia, watu wasiwasikilize wanasiasa uchwara, wananchi wawe na subira kuhusu suala hili,” alisema Makamba.

Julai mwaka huu katika kikao chake cha bajeti, Bunge lilipitisha sheria ya kodi ya tozo ya kadi ya simu ya Sh 1000 kwa kila laini ya simu ya mkononi kwa mwezi, kodi ambayo imelalamikiwa na wananchi kuwa ni kubwa.

Hata hivyo, Rais Jakaya Kikwete, ameingilia kati suala hilo ambapo ameziagiza Wizara za Serikali zinazohusika na kodi na mawasiliano pamoja na kampuni za simu za mikononi nchini, kukutana mara moja kutafuta jinsi gani ya kumaliza mvutano wa kodi mpya ya kadi za simu hizo za mikononi.

0 comments:

Post a Comment